Monday, 29 June 2015

SAFARI ZA UHAMASISHAJI UTALII WA NDANI MSIMU WA SABASABA JUNE 27 HADI JULY 7, 2015

Safari hizi zitafanyika kwa hifadhi za Mikumi na Saadani wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara "Saba saba" kuanzia tarehe 1 hadi 7 July 2015.

 UTARATIBU UTAKUWA KAMA IFUATAVYO
  • Safari zitaanza ijumaa tarehe 3 hadi jumanne tarehe 7 Julai 2015
  • Kutakuwa na safari za aina mbili- za kutwa (go and return) na za kulala (over night) katika hifadhi zote za Mikumi na Saadani.
  • Kwa safari za kutwa (day trips -go and return) wakubwa watalipa Tsh 20,000 na watoto Tsh 10,000. Hii itahusisha gharama ya kwenda, kiingilio, mwongoza wageni, kutalii na kurudi
  • Safari za kulala gharama yake ni  Tsh 35,000 (watoto), Tsh 60,000 (watu wazima) kwa Saadani. Tsh50,000 single au Tsh 60,000 double kwa Mikumi. Hii ni pamoja na usafiri kwenda na kurudi, malazi, chakula cha usiku na chai asubuhi.
  • Saadani kutakuwa na Safari za boti ambazo gharama yake ni Tsh 25,000  (watoto) na Tsh 45,000 (watu wazima) ikijumuisha usafiri kwenda na kurudi pamoja na utalii wa boti.
  • Safari zote hizi zitaanzia Dar es Salaam na kuishia Dar es Salaam: Kwa wanaokwenda Saadani Kituo ni Mwenge (kituo cha mafuta), kwa wanaokwenda Mikumi kituo ni Kimara (Bahama mama) na Sabasaba.
  • Muda wa kuondoka kwa wale wa safari za kutwa ni saa 12.00 alfajiri na kurudi jioni siku hiyo hiyo. Kwa wale wanaokwenda kulala wataondoka saa 9.00 alasiri na kurudi siku inayofuata.
  • Tafadhali zingatia muda, ukichelewa fedha haitarejeshwa.
  • Karibu ufurahie mandhari nzuri, ndege wazuri na wanyama wa kuvutia ambao nchi yetu imejaliwa na mwenyezi Mungu


MPANGILIO WA SAFARI
TAREHE HIFADHI
IDADI YA MAGARI/TRIP
IDADI YA WATALII WA NDANI KILA  SIKU
3.7.2015 MIKUMI
1
20     for over night (kulala)
SAADANI
1
10     for over night (kulala)

4.7.2015
MIKUMI
1
28
SAADANI
1
28

5.7.2015
MIKUMI
1
28
SAADANI
2
56

6.7.2015
MIKUMI
2
56
SAADANI
3
84

7.7.2015
MIKUMI
4
110
SAADANI
4
112
JUMLA
20
532

JINSI  YA KUJIANDIKISHA
Tembelea banda la TANAPA lililopo ndani ya jengo la Wizara ya Mali Asili na Utalii katika viwanja vya Saba Saba kuanzia tarehe 28 Juni hadi 6 Julai 2015.
Zingatia: WAHI MAPEMA, NAFASI NI CHACHE.
UKICHELEWA SAFARI PESA HAIRUDISHWI
 
IMETOLEWA NA IDARA YA MASOKO
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
S.L.P 3134
ARUSHA, TANZANIA

No comments:

Post a Comment