Saturday, 27 June 2015

SERIKALI YA MAREKANI YAZINDUA MRADI WA DOLA MILIONI 14.5 WA KULINDA MAZINGIRA, KUKUZA UHIFADHI NA UTALII NCHINI TANZANIA

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa PROTECT wa dola za kimarekani Milioni 14.5 wa kulinda mazingira, kukuza uhifadhi na utalii nchini hapa unaolenga kujenga uwezo wa uhifadhi na kukabiliana na ujangili na usafirishaji haramu wa wanyamapori nchini kote Tanzania,uzinduzi huu ulifanyika jana katika eneo la hifadhi ya wanyamapori linalosimamiwa na jumuiya ya uhifadhi ya wanyamapori {WMA} la Randilen linalopakana na hifadhi ya taifa Tarangire Wilayani Monduli mkoani Arusha. (Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog).


Na Pamela Mollel, Arusha

Serikali ya Marekani kwa kupitia shirika la ushirikiano wa kimataifa (USAID) imezindua rasmi mradi wa miaka mitano wa kulinda mazingira na kukuza uhifadhi wa utalii wa dolla za kimarekani milioni14.5 hapa nchini ujulikanao kama PROTECT=PROJECT.

Uzinduzi huu ambao umefanyika ndani ya eneo la hifadhi ya wanyamapori linalosimamiwa na jumuiya ya uhifadhi ya wanyamapori (WMA) la Randilen linalopakana na hifadhi ya taifa tarangire Wilayani Monduli mkoani Arusha, Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress amesema mradi huu unalenga kujenga uwezo wa uhifadhi na kukabiliana na ujangili na usafirishaji haramu wa wanyamapori nchini kote Tanzania.

Balozi Mark amesema mradi wa PROTECT utalenga kutoa ufumbuzi wa muda mfupi kwa tatizo kubwa lililopo sasa la ujangili huku likiweka misingi ya mafanikioya muda mrefu katika vita dhidi ya ujangili sanjari na kuhimiza ushirikiano kati ya jumuiya za kiraia.

Amesema mradi huu pia utatoa ruzuku ya miaka mitano ya dola za kimarekani 2.75 milioni kwa jamii inayozunguka hifadhi kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kusimamia raslimali hizo.

Aidha balozi ametangaza mradi mpya wa dola 14 milioni za kimarekani unaotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni utakaoshughulikia maeneo ya bayoanuai zilizopo katika hatari ya kutoweka katika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania utakao fahamika kama Endangered Ecosystems Northern Tanzania project kwa lengo la kupambana na ujangili. kutoa msaada ya moja kwa moja kwa MWA ,jamii na wadau katika sekta ya utalii ili kuboresha usimamizi wa wanyamapori.

Kwa upande wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu baada ya uzinduzi na kusaini mkataba amesema kumekuwa na uvamizi mkubwa katika maeneo ya hifadhi za taifa na kusema kuna mpango makakati wa kuhakikisha njia zote zinafunguliwa ili kuwezesha wanyamapori wote kuwa huru kuzunguka katika hifadhi zote nchini.

Pia amewataka wana jamii wa maeneo ya hifadhi ya jumuiya ya WMA Randilen kukaa na uongozi wa hifadhi na kutatua changamoto zilizopo.

Cultural celebration in Africa – Haydom Cultural Centre-Manyara: Tanzania



4th HAYDOM CULTURAL FESTIVAL-2015
Venue: Haydom Cultural Centre-Manyara: Tanzania
Being one of unique and Africa’s number one cultural festival annually held in rural areas while attracting thousands of local and international visitors, this is a never miss cultural festival on planet Earth.
The Haydom community welcomes the world to it’s highly praised cultural celebration in Africa. The event is held in rural Africa and brings together the four main language groups of the continent to celebrate their cultural values including the traditional artifacts shows, traditional dance performances and competition, cultural film shows, archery competitions, and half marathon just to mention a few. The event also gives visitors an opportunity to taste traditional cuisines, local beers & wines and share your life with local families in camping and professionally organized home-stay programmes
The main tribes that participate includes the Datoga representing the Nilotic group originally from Nile river, Central & Northern parts of Africa, Hadza representing the Khoisans from Eastern and Southern Africa, Iraqw representing the Cushites originally from the Horn of Africa and off-course the largest group of Bantu speaking tribes originally from West Africa been represented by Nyiramba, Nyisanzu and Wagogo just to mention a few
Tourists planning a trip to Northern Tanzania can perfectly include this on their itinerary when exploring popular parks like Serengeti, Kilimanjaro, Tarangire and Lake Manyara National parks without forgetting the majestic Ngorongoro crater.
While in Haydom visitors can embark on professionally organized cultural tours to the Land of Hadzabe-Yaeda Valley territory, visit Datoga, Iraqw and Bantu tribes (Nyisanzu & Nyiramba), explore the Rock art paints, Lake Bassotu (canoeing & fishing), Crater lakes, Mount Hanang, Mulbadow wheat farms, visit the Haydom hospital and the rest of the village.
EXHIBITION:
The Festival attracts a big number of local and international audiences. Companies, individuals and institutions always get a platform for exhibition to display their products
The event plan and organization provides smooth interface between the exhibitors and the audience
Our Culture,…Our Heritage! …Let’s Celebrate
Never miss!
For more information please contact:
Tanzania Tourist Board-Cultural Tourism Programme office in Arusha
Museum Buildings, Boma Road -Arusha
Tel: +255 27 2050025
Cell: +255 786703010
E-mail: culturaltourism@habari.co.tz or ematuro@tanzaniatourism.go.tz
OR
Haydom Four Corners Cultural Programme
Cell: + 255 784238225/762395424
E-mail: amanipaulit@gmail.com Website: www.4ccp.org